fbpx

COVID-19 kwa Swahili

Pata taarifa muhimu zaidi kuhusu COVID-19 kutoka kwa wizara ya afya na serikari ya denmark kwa lugha ya kiswahili

COVID-19 kwa Swahili

Pata taarifa muhimu zaidi kuhusu COVID-19 kutoka kwa wizara ya afya na serikari ya denmark kwa lugha ya kiswahili

RSS
ATOM


Ufunguzi wa Denmark awamu ya tatu

Kuanzia jumatatu tarehe 8 juni 2020, Denmark itafungua tena sehemu zaidi. Hii itajumuisha:

 • Vitengo za michezo za ndani-(michezo za video), mabwawa ya kuogelea na maeneo ya kucheza na kuoga
 • Kumbi za michezo,vituo vya mazoezi na fitness center
 • Viwanja vya nje vya maburudisho – kwa kuzingatia vizuizi maalum kwa hivi viwanja
 • Mipangilio au shughuli za watoto na vijana msimu wa likizo ya summer 
 • Harusi na karamu kubwa- ambazo zina uwezo wa kukusanya hadi watu 500 kwa kuzingatia sheria maalum, ikiwa itafanyika katika mikahawa ambayo itaandaa chakula. Walakini hairuhisiwi wewe mwenyewe kukodisha nyumba na kukusanyika watu 500.
 • Mikutano, mikutano ya baraza- wako tena na uwezo wa kukusanyika hadi watu 500 chini ya hali maalum
 • Ligi kuu, mpira wa miguu – wako na uwezo tena wa kukusanyika hadi watu 500 chini ya hali maalum.

Marufuku ya mikutano ya watu 10 yatafutiliwa mbali kuanzia tarehe 8 juni, na kuanzia tarehe hio nane juni, wameongeza kiwango ya watu ambao wanaweza kukutana pamoja hadi watu 50.

Serikali inatumaini kuongeza uwezo wa watu kukusanyika pamoja hadi watu 100 kuanzia tarehe 8 julai, na hadi watu 200 kuanzia tarehe 8 agosti . Hili ni tumaini tu, bado haijapitishwa.

Tofauti kati ya mikoa

Kwa kuwa kuna tofauti katika maambukizi kati ya mikoa, vile vile kutakuwa na tofauti kati ya mikoa jinsi ufunguzi utakavyo endelezwa. Kwa mfano wafanyakazi wote katika mkoa wa Storebælt kwa sasa wanao uwezo wa kukutana katika sehemu zao za kazi. Walakini huduma za uma katika mkoa wa Sjælland na mji mkuu wanatarajiwa kufungua tena uwezo wa kukutana kazini tarehe 15 juni. 

Støt Mino Danmarks arbejde.


Mipaka imefunguliwa kwa kiwango kidogo, lakini unashauriwa kutosafiri nje ya nchi

Muhutasari wa mkutano kwa waandishi wa habari kutoka kwa waziri Mkuu, tarehe 29 mai 2020

Serikali imetoa ushauri wa kutosafari nje ya nchi hadi tarehe 31 Agosti. Nchi za Norway, Island na ujerumani haijumuishwi katika ushauri huu.

Kuanzia tarehe 15 Juni, Denmark itafungua mipaka kwa wageni kutoka Norway, Island na ujerumani. Walakini kutakuwa na masharti kadha kwa watalii ambao wanatoka katika hizi nchi. Kwa mfano, itawalazimisha wakomboe nyumba ya kulala kiwango ya chini ikiwa usiku sita denmark ili wapewe kibali ya kuiinga nchini na hawatapata ruhusa ya kulala mji mkuu. Vile vile, watafanyiwa upimaji mipakani.

Mpaka kati ya Denmark na Sweden itabaki imefungwa kwa muda kwa sababu nchi ya Uswidi ilitumia njia tofauti ya kukabiliana na janga la virusi vya corona.

Baada ya likizo ya summer, wataangazia ufunguzi wa nchi zingine za Schengen.

Tabia na mienendo yetu ya kila siku itachangia kwa ukubwa vipi ufunguzi wa jamii itakavyoendeshwa. Haya yanajumuisha pia miendendo na tabia zetu tunaposafiri msimu wa likizo ya summer.

Ukisafiri katika nchi zingine una hatari ya kuambukizwa na kuleta maambukizi nyumbani. Kwa hivyo unashauriwa kutosafiri kwa miji mikubwa, na pia kuwa makini na kupata habari juu ya mji unayosafiri na sheria zilizowekwa.

Wizara ya afya inakuhimiza pia ujitenge kwa siku 14 baada ya safari yako ya nchi za ng’ambo, hata kama umekuwa kwa safari fupi nchini Sweden.

Støt Mino Danmarks arbejde.


Sasa unauwezo mwenyewe wa kupata muda wa kupimwa virusi vya corona- hata ikiwa hauna dalili

Sio lazima tena kupata rufaa kutoka kwa daktari wako ili uwe na uwezo wa kupata muda wa kupimwa virusi vya corona. Kuanzia wiki hii wananchi wote hapa denmark wanauwezo wa kupata muda wa upimaji kwa www.coronaprover.dk. Unachohitaji ni kitambulisho yako ya Nem-ID.

Haya yametangazwa na wizara ya afya.

Unaweza kuhifadhi muda wa kupimwa mwenyewe, haijalishi kama upo na dalili au la. Mara tu unapopewa muda, upimaji utatendeka katika moja wapo za hema nyeupe ambazo zimejengwa kwa kusudi hii nchini kote.

Wizara ya afya inakukumbusha kwamba, kama matokeo ya upimaji yanaonyesha kwamba hauna virusi vya corona, haimaanishi kwamba uwache kutimiza miongozo ya kukaa mbali mbali na usafi. Jaribio haiwezi aminika kwa asilia 100%, na kunaweza kuwa na visa ambapo virusi havigundulikani na kipimo, hata ingawa mtu ameambukizwa.

Pata malelezo zaidi hapa https://www.dr.dk/nyheder/indland/nu-kan-alle-danskere-blive-coronatestet

Støt Mino Danmarks arbejde.


Serikali inawasilisha mkakati mpya wa kupima na kufuatilia wale walio ambukizwa

Muhutasari wa mkutano kwa waandishi wa habari kutoka kwa waziri Mkuu, tarehe 12 mai 2020

Hivi karibuni Denmark imeongeza sana, na kwa ukubwa zaidi upimaji wa COVID-19 na kwa sasa hivi ni moja ya nchi ulimwenguni ambayo inapima watu wengi kulingana na idada ya wakaazi nchini. Lakini tunahitaji kuwa bora zaidi kwa sababu ikiwa maambukizi yanaibuka tena ni muhimu kubainiwa kwa wakati unaofaa. Kwa hivyo ni muhimu tuwe na njia dhabiti ya kufuatilia kuenea kwa maambukizi.

Kuna haja ya kuwatenga wagonjwa ili tuweze kuzuia maambukizi zaidi bila kufunga jamii yetu tena. Kwa wakati huo huo, kuna haja ya kuhakikisha kwamba watu wazee na walio katika hatari ya maambukizi pia wawe na uwezo wa kupata uhuru kwa maisha ya kila siku na wawe na uwezo wa kuwaona watoto and wajukuu wao tena.

Mikakati mipya ya ugunduzi na ufuatiliaji bora wa maambukizi inajumuisha: Mtu anapopatikana ameambukizwa, wiki hio, mamlaka inayo wajibika wataanza kutafuta ni nani ambaye umewasiliana naye kwa karibu . Watu hawa wanaweza kupimwa na kutengwa haraka kabla ya maambukizi haya kuenea zaidi. Serikali inaanzisha nambari ya hotline, ambayo itasaidia walioambukizwa kuwatambua wale walio wasiliana nao, kuhakisha na kukomesha kuenea kwa maaambukizi.

Juu ya hayo, serikali kwa mashirikiano na manisipaa watatenga vituo/vymba vya kujitenga kwa wananchi ambao hawana uwezo wa kujitenga kwa nyumba zao.

Støt Mino Danmarks arbejde.


Mamlaka ya teknolojia na usalama inatoa onyo dhidi ya barakoa zinazotengenezwa nyumbani

Watu binafsi wameanza kushona na kutengeneza barakoa wenyewe nyumbani. Walakini barakoa zinazo shonwa hapo nyumbani zinafanya mtu ajihisi yuko salama, na hio sio ukweli, hili ni onyo kali kutoka kwa mamlaka ya teknolojia na usalama.

Usalama usio wa kweli waweza kufanya mtu ajihisi amejikinga na kwa hivyo kutozingatia ushauri kuhusu usafi bora na kukaa mbali mbali. Barakoa iliyo tengenezwa nyumbani haikingi dhidi ya maambukizi ya magonjwa kama COVID-19, kwani chembe chembe za virusi zinaweza kupenya.

Vifaa kama vile barakoa lazima zitimize mahitaji fulani ya kiufundi ili kutoa kinga dhidi ya magonjwa.Kama mtumizi wa vifaa hivi, unaweza kuangalia na kuhakihisha kwamba barakoa unatotumia iko na alama ambayo inaonekana vyema ya ’CE’, ambayo ni alama ya udhibitisho inayoonyesha kwamba kifaa unachotumia imetengenezwa kwa kufuatia maagizo kwa vifaa vya kinga.

Uuzaji wa vifaa vya kinga vilivyo tengenezwa nyumbani na ambavyo havikidhi mahitaji ya sheria ni kinyume cha sheria.

Shirika la usalama wa kitaifa inasisitiza kwamba unapaswa kufuata mapendekezo ya kukaa mbali mbali na usafi bora kama msingi kuu wa kuzuia maambukizo dhidi ya COVID-19.

Pata maelezo zaidi hapa: https://www.sik.dk/erhverv/produkter/personlige-vaernemidler/vejledninger-forbindelse-corona-covid-19/hjemmestrikkede-masker-giver-formentlig-ikke-beskyttelse#

na hapa: https://www.dr.dk/nyheder/indland/styrelse-hjemmestrikkede-og-hjemmesyede-masker-giver-falsk-beskyttelse

Støt Mino Danmarks arbejde.


Awamu ya 2 kufungua denmark upya inaaza sasa

Muhutasari wa mkutano kwa waandishi wa habari tarehe 7 Mei , kutoka kwa Waziri Mkuu Mette Frederiksen

Wananchi wote hapa denmark wamefuata miongozo ya mamlaka juu ya kukaa mbali mbali,kuzingatia usafi bora na kadhalika. Kwa hivyo kwa sasa inawezekana kuendelea na ufunguzi wa taratibu wa shuguli za kila siku hapa denmark. Walakini , miongozo ya mamlaka ya afya kuhusu kukaa mbali mbali na kuwa na usafi bora bado itatimizwa kwa mafanikio ya kufungua tena, ni muhimu miongozo hizi ziendelee kutimizwa.

Mbali na miongozo inayojulikana kwa sasa, kufungua upya itatendeka sambamba na mikakati ya upimaji. Kwa sasa kuna lengo kuu ya upimaji wa dalili, hata ikiwa ni dalili ndogo, kufuatilia maambukizi na kutenga walio ambukizwa. Juu ya hayo, upimaji utatendeka kwa uwakilishaji wa umma,ambapo idadi ya watu watateuliwa na kuitwa kupimwa ikiwa wako na dalili za maambukizi au la.

Awamu ya pili ya kufungua tena ni pamoja na:

· Ufunguzi kamili wa maduka za reja reja, hizi ni pamoja na maduka makubwa ya storcenter (kuanzia tarehe 11 Mei)

· Hoteli, mikahawa na maduka kama haya zinaweza kutumika kwa kuzingatia miongozo maalum ya kuwa mbali mbali na kadhalika (kuanzia tarehe 18 Mei)

· Watoto wa darasa la 6 hadi 10 wanaweza kwenda shule tena (kuanzia tarehe 18 Mei)

· Kampuni za kibinafsu zinaweza kufungua tena kwa mikutano na mahudhurio ya wafanyikazi

· Michezo za kitaalam zinaweza tendeka lakini ifanyike bila ya watazamaji

· Maktaba yatafunguliwa kwa mkopo wa vitabu (kuanzia tarehe 18 Mei)

· Michezo ya nje- mazoezi na vilabu vya nje vinaweza kufungua tena kwa kuzingatia ushauri na kanuni ya afya.

· Makanisa ya Folkekirke na makanisa na dini zingine zafunguliwa kwa kuzingatia ushauri na kanuni ya afya bora (kuanzia tarehe 18 mei)

Kwa sasa uamuzi haujafanywa kuhusu lini udhibiti wa mpaka kwa muda utakoma. Serikali itatatoa ujumbe ifikapi tarehe 1 juni 2020.

Ikiwa kufungua tena kunasababisha janga la corona kuibuka, basi ufunguzi utapunguzwa tena. Mfumo wa utunzaji wa afya ni lazima uwe na uwezo wa kutoa tiba bora kwa kila mmoja katika miezi ijayo.

Soma zaidi katika https://www.regeringen.dk/nyheder/2020/pressemoede-om-genaabning-af-danmark-fase-2/

Støt Mino Danmarks arbejde.


Wizara ya afya imebadilisha ufafanuzi wa ’vikundi vya watu walio hatarini’

Baada ya kufanya kazi na ufafanuzi mpana sana wa vikundi vya watu walio hatarini kwa maambukizi ya COVID-19, Wizara ya afya sasa imefafanua wazi , ni vikundi vipi ambavyo viko kwenye hatari ya kuugua zaidi wakiambukizwa na virusi vya homa kali ya mapavu ya corona.

Sasa kuna vikundi 7 vilivyo hatarini:

1.Watu wazee kwa umri- kulingana na hali yao ya afya kwa jumla

Kulingana na uzoefu ambao tumeona kwa sasa na virusi vya corona, watu zaidi ya miaka 70, na haswa watu zaidi ya miaka 80 wako katika hatari kubwa ya kuwa wagonjwa zaidi. Watu wa miaka 65 na vijana wadogo wako hatarini hasa ikiwa wana ugonjwa sugu moja au zaidi.

Watu wazee wa miaka 65 na zaidi hawazingatiwi moja kwa moja kuwa katika kikundi hatarini ikiwa ni wazima wa afya na wanafanya mazoezi. Inamaanisha pia kuwa babu na nyanya wanaweza kuwaona na kuwakumbatia wajukuu wao walio wazima wa afya.

2.Wakaazi wa nyumba ya watu wazee

Wakaazi wa nyumba ya watu wazee mara nyingi ni watu wazee sana, wana magonjwa sugu na viwango vyao vya mazoezi vimepungua. Kwa hivyo wako katika kikundi ya watu hatarini.

3.Watu walio na uzito mkuu

Watu walio na uzito zaidi ya kawaida mara nyingi huwa na magonjwa sugu kama vile ugonjwa wa sukari au ugonjwa wa moyo. Hasa watu walio na BMI zaidi ya 35, au BMI zaidi ya 30 pamoja na kuwa na ugonjwa sugu wako hatarini ya kuwa wagonjwa zaidi wakiambukizwa na COVID-19.

4.Watu walio na magonjwa sugu

Sio magonjwa yote sugu yanamaana kuwa mtu ako katika kikundi hatari, haswa ikiwa umetibiwa vizuri. Unaweza kupata orodha ya magonjwa ambayo mtu ako hatarini ya kuwa mugonjwa zaidi akiambukizwa na COVID-19, hapa:

https://www.sst.dk/da/Udgivelser/2020/Personer-med-oeget-risiko-ved-COVID-19

5.Watoto fulani walio na magonjwa sugu

Watoto wengine walio na ugonjwa sugu wanaweza kuwa katika hatari kubwa wakiambukizwa na COVID-19. Hao ni watoto ambao tayari wana magonjwa ambayo hayahusiani na janga la virusi ya corona. Wako na malezi tofauti kwa mfano masomo au utunzaji maalum. Watoto hawa na familia zao watapata ushauri wa kibinafsi mahala pao pa matibabu.

6.Watu bila makazi

Watu wasio na makao ya kudumu mara nyingi hawana uwezo wa kudumisha afya bora au kukaa mbali mbali na watu wengine. Kwa hivyo, inasababisha hatari ya uongezevu wa maambukizi.  Zaidi ya hayo, watu wengi bila makao ya kudumu wanakabiliana na magonjwa sugu. Mchanganyiko huu huwafanya wawe katika hatari kubwa ya kuwa wagonjwa zaidi wakiambukizwa na magonjwa.

7.Mama mjamzito

Kwa kuzingatia kanuni ya tahadhari mama mjamizito yuko kwa kikundi ya watu hatarini, kwani kwa ujumla wanawake wajawazito wanaambukizwa magonjwa kwa urahisi.  Hakuna ushahidi kwa sasa kwamba mama mjamzito au mtoto aliye tumboni  ako katika hatari ya kuugua zaidi kuliko watu wengine. Walakini inaonekana kwamba wanawake wajawazito walio lazwa hospitalini kwa maambukizi ya COVID-19, na wako katika trimester ya tatu ya mimba watazalishwa kabla ya siku ya kujifungua kupitia upasuaji. Juu ya hayo, kuna hatari za kawaida kwa mama aliyezaa na mtoto mchanga.

https://www.sst.dk/da/corona/Saerlige-risikogrupper

Støt Mino Danmarks arbejde.


Kwa sasa, vikundi vilivyochaguliwa vya watu walio katika hatari kubwa ya maambukizi watapata chanjo ya bure kwa ugonjwa wa nimonia

Watu walio katika hatari kubwa ya kuwa wagonjwa zaidi kwa maambukizo ya COVID-19, kwa sasa wanaweza kuwasiliana na daktari wao ili wapate chanjo ya bure ya kuzuia nimonia.

Chanjo hii inatolewa kwa vikundi vya watu walio hatarini ili kupunguza hatari ya kuathiriwa na maambukizo mabaya, kwa kuzingatia kwamba watu hawa wako katika hatari ya maambukizi ya COVID-19.

Chanjo inayotolewa kwa vikundi maalum sio chanjo dhidi ya COVID-19. Ni chanjo dhidi ya magonjwa ya bakteria ya nimonia ambayo inaweza kuwa na madhara mbaya na kusababisha hali mbaya zaidi kama vile maambukizi ya damu na mapavu.

Watu wengine wako kwenye hatari kubwa kuliko wengine kwa sababu ya umri wao au kwa sababu wanaugua magonjwa mengine. Kwa hivyo kwa mara ya kwanza, watu ambao wanakaa kwa nyumba ya watu wazee, watu walio na miaka 65 na zaidi na wenye magonjwa sugu, na watu walio chini ya umri 65 walio katika hatari kubwa ya kupata magonjwa na kuwa wagonjwa zaidi ndio watapokea chanjo.

Ili kujua kama uko hatika kikundi hatari na kwa hivo unaweza kupata chanjo ya bure, pata maelezo zaidi hapa:
https://www.sst.dk/da/Viden/Vaccination/

Unaweza kusoma zaidi kuhusu chanjo hapa:
https://www.sst.dk/da

Støt Mino Danmarks arbejde.


Muhtasari wa mkutano kwa waandishi wa habari kutoka kwa waziri wa afya na mamlaka ya afya, tarehe 20 aprili 2020

Tuko katika hatua ya kwanza ya kufunga tena jamii yetu na shughuli za kila siku. Hii ni kwa sababu tumepata kudhibiti janga la magonjwa hapa Denmark. Kufunguliwa upya kunamaanisha kuwa watu zaidi watakuwa wanawasiliana pamoja. Kwa hivyo ufunguzi unaenda sambamba na watu wengi kupimwa, na
wakati huo ni lazima tufuate miongozo ambayo tunazijua kwa sasa ambayo ni pamoja na; kuosha mikono, kukohoa na kupiga chafya katika kiwiko cha mikono, kupunguza mawasiliano ya mwili, kukaa nyumbani ukiwa na magonjwa na uwe makini zaidi na mahala ambapo watu wengi wanatumia.

Tumejitahidi ili tuwe nauwezo na mitambo zaidi ya upimaji, na tuko nayo hivi sasa. Hiyo inamaanisha kwamba watu WOTE, ambao wana dalili wanapaswa kupimwa. Inamaanisha kwamba ikiwa una moja au zaidi ya dalili zifuatazo: kikohozi kavu, homa/mwili kupanda joto au tatizo ya kupumua, unaweza kupimwa kwa virusi vya corona. Unapaswa kupiga simu kwa daktari wako, na ikiwa ni nje ya wakati wa kazi, piga simu kwa daktari anayewajibika (lægevagt), ambapo atafanya mipangilio ili upate kupimwa haraka iwezekanavyo. Hii ni njia bora zaidi ambayo tunaweza kusimamisha maambukizi ya virusi vya corona.
Kumekuwa na wasiwasi kwamba, watu wachache wanawasiliana na daktari wao. Tunawahimiza watu wawasiliane na daktari wao wakiwa wagonjwa au wako na dalili za ugonjwa, haijalishi kama ni magonjwa mengine au magonjwa yanayohusiana na virusi vya corona.

Maelezo ya jumla kuhusu upimaji:

Mtu anapimwa kwa kuchukua sampuli kwa pamba, kupitia mdomo au pua. Ikiwa umelazwa hospitalini na haiwezekani kupimwa kupitia pamba ya mdomo au pua, wataalam watatumia njia nyingine ya kuingiza kipimo la bomba ndogo kwa pua. Upimaji unategemea mambo kadhaa, na mara nyingine inahitajika
kupimwa zaidi ya mara moja.

Støt Mino Danmarks arbejde.


Muhtasari wa mkutano kwa waandishi wa habari kutoka kwa Waziri Mkuu tarehe 14 aprili 2020

Kwa sasa tunaweza kufurahia vile maendeleo ya virusi vya corona inavyo onyesha hapa nchini Denmark. Nambari zinaendelea kuwa zaidi na ilivyo tarajiwa. Kwa hivyo tunaweza kufungua zaidi kidogo kulingana na matarajiwa ya hapo awali. Kutakuwa na majadiliano kati ya vyama tofaututi bungeni kuhusu vitengo vipi vinaweza kufunguliwa zaidi, kwa mfano kazi gani na zipi zinaweza kufunguliwa.
Idadi ya watu ambao wamelazwa hospitalini na kwa vitengo maalum imepungua. Maagizo ya kukaa mbali mbali imefaulu, na ndio maana sote lazima tuendelee vivyo hivyo. Imekuwa jambo lisilo la kawaida, na limeshangaza sisi sote kwamba Denmark imefunga shughuli za kila siku. Lakini nchi zingine nyingi ulimwenguni ziko katika hali ngumu zaidi kuliko Denmark.
Kwa hivi sasa, kuna watu 380 walio lazwa hospitalini na virusi vya homa kali ya mapavu ya corona, watu 93 wamelazwa katika vitengo vya utunzaji maalum, na watu 299 wameaga dunia. Virusi vya Corona vimedhibitiwa nchini denmark kwa sasa na mfumo wa afya unauwezo wa kuendelea kutoa huduma bora.

 • Maandalio sasa yanafanyiwa ili kufungua sehemu zingine za mfumo wa huduma ya afya ili madaktari wa kibinafsi wawe na uwezo wa kutibu wagonjwa na hospitali pia zinaweza kuanza kufanya mipango ya upasuaji/matibabu ya operation. Wagonjwa walio na mahitaji makubwa zaidi watapewa muda kwanza. Kila mtu akumbuke kuwasiliana na daktari wake wa kibinafsi ukiwa mgonjwa, au dalili za magonjwa na unahitaji uchunguzi zaidi.
 • Manisipaa (kommune) zote zinajiandaa kufungua tena taasisi za utunjazi na malezi
 • (daginstitutioner, dagplejer) na shule kwa msingi wa mapendekezo kutoka kwa wizara ya afya. Maisha ya kila siku itakuwa tofauti kwa watoto, kwani wanapaswa kukaa mbali mbali kati yao, na watatumia muda zaidi nje na kucheza kwa vikundi vidogo vidogo.
 • Manisipaa (kommune) 67 wanafungua huduma za shule kesho, jumatano 15 aprili 2020 na manisipaa 48 wanafungua shule darasa la sufuri hadi tano, ijumaa tarehe 17.april 2020. Taasisi zingine zote za utunzaji na malezi ya watoto pamoja na shule za msingi zitafungua jumatatu tarehe 20 aprili 2020.

Lazima tuendelee na tutilie maanani kuwa mbali mbali na kuwalinda watu wazee na walio katika hatari kubwa ya maambukizi katika jamii. Sisi sote tunahitaji kusaidia ili maambukuzi hayaenei sana na kwa haraka.

Støt Mino Danmarks arbejde.


Muhtasari wa mkutano kwa waandishi wa habari kutoka kwa Waziri Mkuu tarehe 6 aprili 2020, saa mbili usiku (Kl.20.00).

Maendeleo ilivyo sasa ni thabiti na nambari zinaendelea sawa: watu 503 wamelazwa hospitalini, watu 139 wamelazwa katika kitengo cha utunzaji maalum, na watu 187 kwa bahati mbaya wameaga dunia.
Waziri mkuu anabainisha kuwa, virusi huhisiwa kwanza baada ya wiki tatu au nne baada ya maambukizo,na kwa hivyo kuna wasiswasi, kuwa watu wengine wataanza kutozingatia maagizo kwa mfano kwa kusherekea pasaka pamoja.
Kwa msingi huo, waziri mkuu amewasilisha mpango ya kwanza, awamu ya kuanza kufungua tena Denmark. Vidokezo vyote vya mipango ni kwa masharti kuwa kila mtu anachukua jukumu na kuendelea kufuata maagizo ya mamlaka: kuosha mikono, na kukaa mbali mbali na kutokutana na watu wengi.

 1. Awamu ya kwanza ya ufunguzi inajumuisha:
 • Huduma ya afya itafunguliwa tena kwa shughuli nyingine mbali na corona.
 • Vituo vya kulea watoto (vuggestuer,børnehaver,SFO) na shule, madarasa ya 0-5 yatafunguliwa tena.
  o Katika taasisi hizi hatua kadhaa mpya za utunzaji zitatumiwa, njia na mwelekeo mpya wa kuzingatia usafi. Ufunguzi utafanyika kwanza, mipangilio haya yakiwa tayari.
 • Wafanyikazi wa kibinafsi kwa kuzingatia maagizo ya afya wataanza kazi tena.

Waziri mkuu anasisitiza kwamba, haya yote ni kwa masharti kwamba, maendeleo yata kuwa thabiti- na kwamba sisi sote tunayo jukumu la kuhakikisha kwamba inawezekana, kwa kufuata miongozo.
Kwa kuongezea, hatua zingine lazima ziongezwe muda kwa wiki nne zaidi hadi tarehe 10 mei.2020, haya yanahusu:

 • Kufungwa kwa mipaka.
 • Kupiga marufuku mukusanyiko zaidi ya watu 10.
 • Miongozo mikali.
 • Masomo ya vio vikuu, maktaba, sinema, maduka makubwa(storcenter), mikahawa zitaendelea kufungwa.
 • Biashara ndogo ndogo kama vile watunzaji wa nywele, tatoo na kadhalika, bado zitafungwa.

Waziri mkuu anahimiza watu wote wawe wavumilivi na kuelewa, hakuna kitu kitakuwa sawa kama hapo awali- na maisha ya kila siku hayatarudi kama kawaida kwa miezi kadhaa.
Kwa kuongezea anatangaza maswala kadhaa kuhusu:

 • Wanafunzi wa darasa la 6-10 wataendelea kuhudhuria masomo wakiwa nyumbani, lakini mitihani ya mwisho wa mwaka imehairishwa na badala yake kupewa matokeo ya mwaka (årskarakter).
 • Wanafunzi wanaomaliza masomo ya sekondari (ungdomsuddanelse), watalazimika kufanya mitihani yao kwa njia tofauti.
 • Sherehe kubwa, masoko ya nje na hafla zingine kubwa katika msimu wa kiangazi (summer) haitawezekana kufanyika . Marufuku ya mikutano mikubwa yataendelea hadi mwezi wa agosti.
 • Serikali na vyama vya bunge vitaangalia ikiwa vifurushi vya misaada
  (hjælpepakkerne) vinaweza kuboreshwa.

Kwa kuongezea waziri mkuu anasisitiza wito wake wa kuonyesha ushikamano na wito wa jamii, wakati huu haswa kwa benki na kampuni kubwa za kukodisha, wanahitajika kuonyesha muungano. Wananchi pia wanahimizwa kuinua uchumi na kukuza biashara na kampuni ndogo.
Kuhusiana na mfumo wa afya, waziri mkuu ametangaza watu wengi wamepimwa, ili kueleza ni watu wangapi ambao wamekuwa na corona, vile vile wanafanya bidii ili kuhakikisha kuwa wafanyakazi wa huduma ya afya wanavyo vifaa vyote vinavyo hitajika.
Mwishowe, waziri mkuu anasema jambo muhimu zaidi ni kwamba sote tunachangia: ni jukumu la kila mtu kufuata maagizo. Haya ndio masharti kwa jamii yetu kufunguliwa tena pole pole.

Støt Mino Danmarks arbejde.


Ushauri kutoka kwa wizara ya afya: Jikinge wewe na wengine dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapavu inayosababishwa na virusi vya corona.

Unachohitaji kujua kuhusu corona:
Hivi sasa tuko katika janga kubwa la maambukizi ya virusi vya homa kali ya CORONA, kwa hivyo ni muhimu kupunguza hatari ya kueneza maambukizi. Wizara ya afya inawahimiza kila mtu kufuata mashauri haya.
Ikiwa wewe ni mzima wa afya:

 • Epuka kuwa karibu na watu wengine, na waombe watu wengine wawe makini.
 • Ikiwa umekuwa karibu na mtu ambaye anaonyesha dalili za homa kali ya virusi ya corona, uwe makini zaidi na dalili zako.
 • Tunza wapendwa wako vyema, na ikiwa wako katika kikundi hatari, uwajali kwa umbali.

Ukiwa na dalili za magonjwa:

 • Kaa nyumbani hadi siku mbili baada ya dalili kupotea
 • Kaa mbali na watu wengine nyumbani, na ukiwa na uwezo kaa kitandani(chumba cha mapumuziko).
 • Uwe mwagalifu zaidi na usafi wa kibinafsi na usafi wa nyumbani.
 • Waulize wengine wakusaidie kwa kununua chakula na uwasiliane nao kwa simu.
 • Ikiwa unahisi dalili zina zidi kuwa mbaya, kwa mfano – kupanda joto mwilini, au matatizo kupumua piga simu kwa daktari.

Jikinge wewe ili ukinge wengine.

Støt Mino Danmarks arbejde.


Serikali inaongeza muda wa kufunga shughuli za kila siku hadi tarehe 13 aprili 2020

Mkutano kwa waandishi wa habari kutoka kwa Waziri mkuu, tarehe 23.03.2020 saa tisa kamili mchana (kl.15.00)


Waziri mkuu Mette Frederiksen ameongeza muda na mipangilio yote kuhusu kudhibitisha magonjwa ya CORONA hadi tarehe 13 aprili 2020.


Watu 254 wamelazwa hospitalini wakiwa na magonjwa ya virusi vya homa kali ya mapavu vya CORONA, watu 55 wamelazwa kwa kitengo cha utunzaji maalum, na watu 24 wameaga dunia.


Mipangilio iliyoamuliwa na bunge hapo mwanzoni, bado itaendelea kutimizwa. Kazi kuu sasa hivi ni kuzuia watu wengi wasiambukizwe na kuwa wangojwa kwa mara moja. Kwa sababu hio, serikali imeongeza muda, na kufunga shughuli za kila siku hadi tarehe 13 aprili 2020.


Waziri mkuu Mette Frederikesen anasisitiza kwamba ni muhimu kila mtu kufuata sheria na mikakati zilizowekwa, kuwa mbali mbali, ingawa inaweza kuwa changa moto wakati wa pasaka. Wana wasihi watu wasisafiri msimu wa pasaka, hata kama ni usafiri wa humu mjini danmark.


Familia zilizo hatarini , lazima watumie utunzaji wa dharura, kwani kuna uwezo wa kutosha wa kutunza watoto na vijana. Vile vile nafasi za nyumba zimetengwa ili watu wasio na makaazi pia waweze kujitenga, ikiwa wataambukizwa.


Waziri wa afya anasema kwamba wanafanya kazi kwa bidii ili kupanua na kuboresha uwezo wa matibabu. Wamewasiliana na Korea kusini kwa ombi na makubaliano ya kununua vifaa vya upimaji.


Kwa kumaliza, waziri wa afya anasema kwamba wanakaribisha na kupokea msaada wowote. Ikiwa kuna mtu anataka kusaidia basi tafadhali pata maelezo zaidi mtandaoni kwa coronasmitte.dk. Hapo utapata kiingilio cha ’Danmark inasaidia Danmark’ ambapo unaweza kupata tathmini ya haraka jinsi unaweza kusaidia.

Støt Mino Danmarks arbejde.


Mama mjamzito mwenye dalili za CORONA lazima apimwe kabla ya kuzaa

Tarehe 19.03.2020, wizara ya afya, imetoa mwongozo mpya kuhusu njia ya kuwatunza mama wajawazito ambao wameambukizwa na COVID-19, mama aliye jifungua, waume/wenzi wao na mtoto aliye zaliwa.
Kuanzia sasa wanawake wote wajawazito wanapofika hospitalini, lazima wapimwe ugonjwa wa homa kali ya mapavu ya virusi vya CORONA.
Majibu yakionyesha kwamba mama mjamzito ameambukizwa , wafanyakazi, wauguzi, daktari na mkunga lazima wachukue tahadhari na kuvaa vifaa muhimu kama barakoa (maske), ili kuzuia kuambukizwa. Mama mjamzito lazima pia naye avae barakoa (maske).
Ikiwa kuna hofu ya kwamba, mtoto aliye zaliwa ameambukizwa na virusi vya homa kali ya mapavu ya CORONA, kwa kutumia kanuni ya uangalifu atatunzwa kama mtu yeyote ambae ameambukizwa hadi matokeo ya majibu yatapo pokelewa.
Zaidi ya hayo:
Mume/mwenzio aliyeambukizwa hakubaliwi kuwa wakati wa kuzaa. Hatakubaliwa vile vile, kuwa wakati wa mtoto anazaliwa akishukiwa kuwa ameambukizwa na virusi vya CORONA.
Mume/mwenzio aliyeambukizwa atakiwa kuwa mbali na mtoto aliyezaliwa, masaa 48 kutoka siku ya mwisho ya dalili hizo.
Hospitali nyingi wakati huu zinahimiza kupunguza kiwango cha jamaa hospitalini. Atakubaliwa pekeyake mume/mwenzio wakati wa kujifungua ili kupunguza uwezekano wa uambukizaji.
Licha ya kwamba mama ameambukuzwa na COVID-19, hatatengwa kutoka kwa mtoto mchanga isipokuwa mama yuko katika hali mbaya ambayo anahitaji matibabu.
Ikiwa majibu yaonyesha kwamba mama ameambukizwa na magonjwa lakini haitaji matibabu , inashauriwa arudi nyumbani kutoka hospitalini haraka iwezekanavyo. Mama atapata maelezo jinsi ya kutunza afya ya mtoto nyumbani.

Støt Mino Danmarks arbejde.


Kutoka kwa Statens Serum Institut, Jumatano 18 Machi.

Wito kwa raia wote.

Taasisi ya Jimbo la Serum inahimiza raia wote kujiandikisha kwa Kuvimba, katika mapambano ya kupiganisha dhidi ya Coronavirus.

Influmeter inategemea juhudi zako za hiari kama raia ambaye, bila kujali umetafuta matibabu au umepokea matibabu, ripoti kila wiki ikiwa una dalili. Kwa kufanya hivyo, unachangia maarifa juu ya usambazaji katika jamii.

Kila mtu anayeishi Denmark anaweza kujiunga na influmeter – watoto, vijana, wazee, wenye afya na wagonjwa. Unaweza kujiandikisha mwenyewe au washiriki wa kaya. Hata kama wewe au wengine tayari kuwa wagonjwa ama mwanzo kuambukizwa Washiriki wote wanachangia habari muhimu kwa wote, wagonjwa, wale ambao wamekuwa na ao wanaweza kuwa. Kwa hivyo usijizuwie hata ikiwa hufikiri kuwa unaugua bado au tayari na kisha kuugua

Idara ya Maambukizo ya Magonjwa ya Kuambukiza, Taasisi ya Serum taifani, inachunguza na kuzuia magonjwa ya kuambukiza nchini Denmark na imefanya kazi zake kama sehemu ya uchunguzi wa ugonjwa mzima kuhusiana na homa ya mafua, homa na dalili za COVID-19

Kutaka elewa mengi nenda influmeter kwa: www.influmeter.dk

Støt Mino Danmarks arbejde.


MUKUTANO KWA WAANDISHI WA HABARI TAREHE 17.03.2020

Waliohudhuria:
Waziri mkuu Mette Frederiksen,Waziri wa afya Magnus Heunicke, Mkurugenzi wa huduma ya afya
Søren Brostrøm, na mwakilishaji kutoka wizara ya uhamiaji na Mkurugenzi wa Polisi Torkild
Fogde.


Waziri mkuu alianza kwa kusisitiza umuhimu vile hali ilivyo kwa sasa, na inaendelea kuwa mbaya.


Watu 82 wamelazwa hospitalini, kati yao, watu 18 wamelazwa katika kitengo cha utunzaji maalum, hii ikiwa mara dufu kwa siku moja. Kwa hivyo ni muhimu tukomeshe maenezi ya haya maambukizi. Mipango mpya inawasilishwa kuanzia kesho tarehe 18.03.2020 saa 10.00 –mchana, hadi tarehe 30.03.2020.

Mikusanyiko ya watu kuzidi 10 imepigwa marufuki, ndani na nje, kwa hafla za umma. Unashauriwa usikusanyike zaidi ya watu 10 kwa mipango au faragha ya kibinafsi.

 • Vikwazo zaidi zimewekwa kuhusu maduka: lazima kuwe na nafasi ya kutosha kati ya watu,
  umbali wa kutosha, wateja wawe na uwezo wa kuaosha mikono, ndani na nje ya maduka.
 • Vituo vyote vya michezo na mazoezi ya ndani vitafungwa, kwa mfano vituo vya mazoezi
  ya gym, duka za kutengeneza nywele, tattoo- Kwa ujumla wafanyaji biashara –kwa sababu
  ya asili ya kazi yao wako karibu na wateja. Haya vikwazo haijumuishi wale ambao
  wanapeana matibabu.
 • Vilabu vya usiku, mikahawa ya kuvuta sigara, (vandpibecafeer) na mastarehe zote lazima
  zifungwe.
 • Vituo vya kuota jua bandia (solcenter),mahala pa kuchezea video (video games)- lakini sio
  maduka ya kuuza vyakula kwa vituo vikuu, lazima zifungwe.
 • Mikahawa,hoteli na kadhalika inapaswa kufungwa- lakini chakula ya kununua na kwenda
  nayo itaendelezwa.
 • Wadanish wote wanaorejea nyumbani kutoka nje ya nchi , wajiaondoe katika orodha
  iliyotengwa , ikiwa wamesajiliwa tena na kwenda nyumbani kwa hiari yao na kujitenga
  kwa siku 14.

  Heunicke, Brørstrøm na Føgde walisisitiza uzito wa hali ilivyo kwa sasa. Ni wakati huu inabidi kuchukua hatua kali ikiwa tunataka kuepuka matokeo mabaya. Hakuna mtu yeyote anayeweza
  kuacha kufuata haya mapendekezo ya wizara ya afya, haya maelezo yakiwalenga haswa, vijana.

  Kama suala la kanuni, waziri mkuu alipendekeza kwamba, ikiwa una shauku juu ya kitu fulani kinachohusiana na afya, kama kwa mfano kula chakula cha jioni pamoja na marafiki, ni heri uache kuhudhuria.
  Waziri mkuu aliwashukuru tena kila mtu ambaye yuko katika kitengo ya maandalizi.

  Kwa kuongezea, waziri mkuu alitangaza vifurushe vipya vya misaada (hjælpepakker), kwa wafanyakazi wanaoajiriwa na waliojiajiri na kwa makampuni. Bunge itajadiliana kuanzia mapema kesho kati ya vyama tofauti. Polisi watapatikana zaidi ya kawaida kwa kuwashauiri na kuwaongoza raia. Wizara ya mambo ya nje inakadiria kuwa kuna wadanish wengi ambao wamekwama nchi za nje, na
  anawashauri kwamba watafute mahala pazuri pa kukaa. Danmark itawaleta nyumbani haraka iwezekanavyo.

Støt Mino Danmarks arbejde.


Rekodi mukutano ya matangazo la chumba cha waziri Mkuu ya taifa ipatikapo: 13 Marts, saa. 19:00

Washariki:
Mwazirimkuu wa taifa: Mette Frederiksen,
Mwaziri la nje: Jeppe Kofoed,
Mwaziri la sheria: Nick Hækkerup
na mkuu wa serikali polisi: Torkild Fogde.

Mwanzo serikali ya Danemark kutoa hali ya virusi-korona Iinchini: kuambukiswa watu: 802, kuazimishwa: 23, hali mbofu: 2. Kisha hapo kuanzisha Mette Frederiksen mwenendo mpya ya kupiganisha kuenea kwa virusi-korona Danemark

Mwanzo – hospitali zinaazimishwa ku acha matibabu zisio za muhimu
; Kwa mfano, shuguli la matibabu ama vipimo vya kawaida, na zisio muhimu sana kuaririshwa.

Ya pili – Waziri la nje ana shauri kwa wote kuto safiri kama si lazma kutoka nje la nchi Danemark kwenda nchi zote zengine na lingine ni ana shauri na kuwaazmisha wanainchi kutoka Denmark waliweko nje kurudi nyumbani haraka iwezekavyo nikusema kama usi safiri nje kama iwezekana kuepuka lakini kama tayari uliko sasa nje ya inchi huko rudia kwa haraka nyumbani

Ya tatu – mpaka hapo inayofikia mbali zaidi – sasa Danemark kutoka kesho Jumamosi tarehe: 14., saa 12:00 imefunga mipaka yake mpaka 14. april. Nikusema itakuwa vigumu wageni kutoka nchi zengine kuingia ndani la nchi Danemark haifati wakija kwa ndege, mashua, treni , Baasi ama gari haiwezekani tena isipokuwa wana ivyo vitambulisho kustahili niya /; Nikusema kwa mfano, wakiishi na kufanya kazi, kwa ziara ya dharura kumuona ndugu mgonjwa sana ama haki za kujiliwa na watoto wake Danemark.
Mipaka zinatekelezwa na polisi na kusaidiwa na askari lakini Serikali inaongeza kwamba viakula maalum vitaendelea kuvuka mipaka bila shida, uhaba usiwe na tena wanainchi bila shaka kuendelea kuingia nyumbani Danemark

Støt Mino Danmarks arbejde.


Samarbejdspartnere til Mino Danmarks indsats med oversættelse af myndighedernes udmeldinger om covid-19 i Danmark:

Vær med til at sikre
et ligeværdigt Danmark
– for alle!

Sammen styrker vi minoritetsetniske danskeres
muligheder, stemmer og samfundsdeltagelseHvert eneste medlemskab og donation styrker Mino Danmarks legitimitet og eksistensberettigelse.

Det gør en forskel og styrker foreningens muligheder for at lykkes med at skabe et lige samfund, uanset etnisk baggrund.

Hvert eneste medlemskab og donation styrker Mino Danmarks legitimitet og eksistensberettigelse.

Det gør en forskel og styrker foreningens muligheder for at lykkes med at skabe et lige samfund, uanset etnisk baggrund.