23/04/2020 /
/Tuko katika hatua ya kwanza ya kufunga tena jamii yetu na shughuli za kila siku. Hii ni kwa sababu tumepata kudhibiti janga la magonjwa hapa Denmark. Kufunguliwa upya kunamaanisha kuwa watu zaidi watakuwa wanawasiliana pamoja. Kwa hivyo ufunguzi unaenda sambamba na watu wengi kupimwa, na
wakati huo ni lazima tufuate miongozo ambayo tunazijua kwa sasa ambayo ni pamoja na; kuosha mikono, kukohoa na kupiga chafya katika kiwiko cha mikono, kupunguza mawasiliano ya mwili, kukaa nyumbani ukiwa na magonjwa na uwe makini zaidi na mahala ambapo watu wengi wanatumia.
Tumejitahidi ili tuwe nauwezo na mitambo zaidi ya upimaji, na tuko nayo hivi sasa. Hiyo inamaanisha kwamba watu WOTE, ambao wana dalili wanapaswa kupimwa. Inamaanisha kwamba ikiwa una moja au zaidi ya dalili zifuatazo: kikohozi kavu, homa/mwili kupanda joto au tatizo ya kupumua, unaweza kupimwa kwa virusi vya corona. Unapaswa kupiga simu kwa daktari wako, na ikiwa ni nje ya wakati wa kazi, piga simu kwa daktari anayewajibika (lægevagt), ambapo atafanya mipangilio ili upate kupimwa haraka iwezekanavyo. Hii ni njia bora zaidi ambayo tunaweza kusimamisha maambukizi ya virusi vya corona.
Kumekuwa na wasiwasi kwamba, watu wachache wanawasiliana na daktari wao. Tunawahimiza watu wawasiliane na daktari wao wakiwa wagonjwa au wako na dalili za ugonjwa, haijalishi kama ni magonjwa mengine au magonjwa yanayohusiana na virusi vya corona.
Maelezo ya jumla kuhusu upimaji:
Mtu anapimwa kwa kuchukua sampuli kwa pamba, kupitia mdomo au pua. Ikiwa umelazwa hospitalini na haiwezekani kupimwa kupitia pamba ya mdomo au pua, wataalam watatumia njia nyingine ya kuingiza kipimo la bomba ndogo kwa pua. Upimaji unategemea mambo kadhaa, na mara nyingine inahitajika
kupimwa zaidi ya mara moja.
08/06/2020
Kuanzia jumatatu tarehe 8 juni 2020, Denmark itafungua tena sehemu zaidi. Hii itajumuisha: Vitengo za michezo za ndani-(michezo za video), […] Læs mere… Læs mere…
29/05/2020
Muhutasari wa mkutano kwa waandishi wa habari kutoka kwa waziri Mkuu, tarehe 29 mai 2020 Serikali imetoa ushauri wa kutosafari […] Læs mere… Læs mere…
19/05/2020
Sio lazima tena kupata rufaa kutoka kwa daktari wako ili uwe na uwezo wa kupata muda wa kupimwa virusi vya […] Læs mere… Læs mere…
13/05/2020
Muhutasari wa mkutano kwa waandishi wa habari kutoka kwa waziri Mkuu, tarehe 12 mai 2020 Hivi karibuni Denmark imeongeza sana, […] Læs mere… Læs mere…
12/05/2020
Watu binafsi wameanza kushona na kutengeneza barakoa wenyewe nyumbani. Walakini barakoa zinazo shonwa hapo nyumbani zinafanya mtu ajihisi yuko salama, […] Læs mere… Læs mere…
07/05/2020
Muhutasari wa mkutano kwa waandishi wa habari tarehe 7 Mei , kutoka kwa Waziri Mkuu Mette Frederiksen Wananchi wote hapa […] Læs mere… Læs mere…
06/05/2020
Baada ya kufanya kazi na ufafanuzi mpana sana wa vikundi vya watu walio hatarini kwa maambukizi ya COVID-19, Wizara ya […] Læs mere… Læs mere…
04/05/2020
Watu walio katika hatari kubwa ya kuwa wagonjwa zaidi kwa maambukizo ya COVID-19, kwa sasa wanaweza kuwasiliana na daktari wao […] Læs mere… Læs mere…
14/04/2020
Kwa sasa tunaweza kufurahia vile maendeleo ya virusi vya corona inavyo onyesha hapa nchini Denmark. Nambari zinaendelea kuwa zaidi na […] Læs mere… Læs mere…
06/04/2020
Maendeleo ilivyo sasa ni thabiti na nambari zinaendelea sawa: watu 503 wamelazwa hospitalini, watu 139 wamelazwa katika kitengo cha utunzaji […] Læs mere… Læs mere…
Hvert eneste medlemskab og donation styrker Mino Danmarks legitimitet og eksistensberettigelse.
Det gør en forskel og styrker foreningens muligheder for at lykkes med at skabe et lige samfund, uanset etnisk baggrund.
Hvert eneste medlemskab og donation styrker Mino Danmarks legitimitet og eksistensberettigelse.
Det gør en forskel og styrker foreningens muligheder for at lykkes med at skabe et lige samfund, uanset etnisk baggrund.