06/05/2020 /
/Baada ya kufanya kazi na ufafanuzi mpana sana wa vikundi vya watu walio hatarini kwa maambukizi ya COVID-19, Wizara ya afya sasa imefafanua wazi , ni vikundi vipi ambavyo viko kwenye hatari ya kuugua zaidi wakiambukizwa na virusi vya homa kali ya mapavu ya corona.
Sasa kuna vikundi 7 vilivyo hatarini:
1.Watu wazee kwa umri- kulingana na hali yao ya afya kwa jumla
Kulingana na uzoefu ambao tumeona kwa sasa na virusi vya corona, watu zaidi ya miaka 70, na haswa watu zaidi ya miaka 80 wako katika hatari kubwa ya kuwa wagonjwa zaidi. Watu wa miaka 65 na vijana wadogo wako hatarini hasa ikiwa wana ugonjwa sugu moja au zaidi.
Watu wazee wa miaka 65 na zaidi hawazingatiwi moja kwa moja kuwa katika kikundi hatarini ikiwa ni wazima wa afya na wanafanya mazoezi. Inamaanisha pia kuwa babu na nyanya wanaweza kuwaona na kuwakumbatia wajukuu wao walio wazima wa afya.
2.Wakaazi wa nyumba ya watu wazee
Wakaazi wa nyumba ya watu wazee mara nyingi ni watu wazee sana, wana magonjwa sugu na viwango vyao vya mazoezi vimepungua. Kwa hivyo wako katika kikundi ya watu hatarini.
3.Watu walio na uzito mkuu
Watu walio na uzito zaidi ya kawaida mara nyingi huwa na magonjwa sugu kama vile ugonjwa wa sukari au ugonjwa wa moyo. Hasa watu walio na BMI zaidi ya 35, au BMI zaidi ya 30 pamoja na kuwa na ugonjwa sugu wako hatarini ya kuwa wagonjwa zaidi wakiambukizwa na COVID-19.
4.Watu walio na magonjwa sugu
Sio magonjwa yote sugu yanamaana kuwa mtu ako katika kikundi hatari, haswa ikiwa umetibiwa vizuri. Unaweza kupata orodha ya magonjwa ambayo mtu ako hatarini ya kuwa mugonjwa zaidi akiambukizwa na COVID-19, hapa:
https://www.sst.dk/da/Udgivelser/2020/Personer-med-oeget-risiko-ved-COVID-19
5.Watoto fulani walio na magonjwa sugu
Watoto wengine walio na ugonjwa sugu wanaweza kuwa katika hatari kubwa wakiambukizwa na COVID-19. Hao ni watoto ambao tayari wana magonjwa ambayo hayahusiani na janga la virusi ya corona. Wako na malezi tofauti kwa mfano masomo au utunzaji maalum. Watoto hawa na familia zao watapata ushauri wa kibinafsi mahala pao pa matibabu.
6.Watu bila makazi
Watu wasio na makao ya kudumu mara nyingi hawana uwezo wa kudumisha afya bora au kukaa mbali mbali na watu wengine. Kwa hivyo, inasababisha hatari ya uongezevu wa maambukizi. Zaidi ya hayo, watu wengi bila makao ya kudumu wanakabiliana na magonjwa sugu. Mchanganyiko huu huwafanya wawe katika hatari kubwa ya kuwa wagonjwa zaidi wakiambukizwa na magonjwa.
7.Mama mjamzito
Kwa kuzingatia kanuni ya tahadhari mama mjamizito yuko kwa kikundi ya watu hatarini, kwani kwa ujumla wanawake wajawazito wanaambukizwa magonjwa kwa urahisi. Hakuna ushahidi kwa sasa kwamba mama mjamzito au mtoto aliye tumboni ako katika hatari ya kuugua zaidi kuliko watu wengine. Walakini inaonekana kwamba wanawake wajawazito walio lazwa hospitalini kwa maambukizi ya COVID-19, na wako katika trimester ya tatu ya mimba watazalishwa kabla ya siku ya kujifungua kupitia upasuaji. Juu ya hayo, kuna hatari za kawaida kwa mama aliyezaa na mtoto mchanga.
08/06/2020
Kuanzia jumatatu tarehe 8 juni 2020, Denmark itafungua tena sehemu zaidi. Hii itajumuisha: Vitengo za michezo za ndani-(michezo za video), […] Læs mere… Læs mere…
29/05/2020
Muhutasari wa mkutano kwa waandishi wa habari kutoka kwa waziri Mkuu, tarehe 29 mai 2020 Serikali imetoa ushauri wa kutosafari […] Læs mere… Læs mere…
19/05/2020
Sio lazima tena kupata rufaa kutoka kwa daktari wako ili uwe na uwezo wa kupata muda wa kupimwa virusi vya […] Læs mere… Læs mere…
13/05/2020
Muhutasari wa mkutano kwa waandishi wa habari kutoka kwa waziri Mkuu, tarehe 12 mai 2020 Hivi karibuni Denmark imeongeza sana, […] Læs mere… Læs mere…
12/05/2020
Watu binafsi wameanza kushona na kutengeneza barakoa wenyewe nyumbani. Walakini barakoa zinazo shonwa hapo nyumbani zinafanya mtu ajihisi yuko salama, […] Læs mere… Læs mere…
07/05/2020
Muhutasari wa mkutano kwa waandishi wa habari tarehe 7 Mei , kutoka kwa Waziri Mkuu Mette Frederiksen Wananchi wote hapa […] Læs mere… Læs mere…
04/05/2020
Watu walio katika hatari kubwa ya kuwa wagonjwa zaidi kwa maambukizo ya COVID-19, kwa sasa wanaweza kuwasiliana na daktari wao […] Læs mere… Læs mere…
23/04/2020
Tuko katika hatua ya kwanza ya kufunga tena jamii yetu na shughuli za kila siku. Hii ni kwa sababu tumepata […] Læs mere… Læs mere…
14/04/2020
Kwa sasa tunaweza kufurahia vile maendeleo ya virusi vya corona inavyo onyesha hapa nchini Denmark. Nambari zinaendelea kuwa zaidi na […] Læs mere… Læs mere…
06/04/2020
Maendeleo ilivyo sasa ni thabiti na nambari zinaendelea sawa: watu 503 wamelazwa hospitalini, watu 139 wamelazwa katika kitengo cha utunzaji […] Læs mere… Læs mere…
Hvert eneste medlemskab og donation styrker Mino Danmarks legitimitet og eksistensberettigelse.
Det gør en forskel og styrker foreningens muligheder for at lykkes med at skabe et lige samfund, uanset etnisk baggrund.
Hvert eneste medlemskab og donation styrker Mino Danmarks legitimitet og eksistensberettigelse.
Det gør en forskel og styrker foreningens muligheder for at lykkes med at skabe et lige samfund, uanset etnisk baggrund.